Huyu Jerry Muro Ana Matatizo Gani Jamani? Angalia Video Jinsi Alivyoropoka Maneno Yaliyowasikitisha Wengi...



Huyu Jerry Muro Ana Matatizo Gani Jamani? Angalia Video Jinsi Alivyoropoka Maneno Yaliyowasikitisha Wengi...
Jerry Muro
Jana katika Press Conference pale Jangwani msemaji wa klabu ya yanga jerry muro hakika alitufanya watu wenye akili zetu tena zilizotukuka tuwe na mashaka nae ya kitaaluma na kiuweledi kutokana na kile alichokifanya ambacho nashukuru hakikumfurahisha kila mtu aliyekuwepo pale na hasa hasa wana Yanga wenzake wale wenye uwezo wa kuchambua masuala.

Hivi ni kweli Jerry Muro anajua majukumu hasa ya afisa habari au afisa uhusiano au meneja mahusiano au kurugenzi ya habari, uhusiano na mawasiliano?

Yaliyonifanya hadi nikaamua kuanzisha huu uzi ni kitendo chake ambacho binafsi naweza kukiita ni kama vile ameibaka taaluma na ikiwezekana upesi na haraka sana atuombe radhi wana taaluma na hapa ndipo tutapima uimara wa uongozi wa klabu ya Yanga kama utamwajibisha au na wenyewe utaungana nae Jerry Muro.

Jana pale mkutanoni Jerry Muro wakati akijibu maswali ya wanahabari, ghafla akapotoka katika hoja ya msingi na kuanza kumjibu hovyo msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Manara.

Na ili muyaamini haya niyasemayo naomba kama una mwandishi yoyote wa habari ambaye jana alikuwepo pale ukumbini, muulize maneno machafu, ya kejeli, kudhalilisha, ya kishamba na sifa ambayo Muro alikuwa akiyasema pale.

Hapa nitayasema kisha nitawaombeni nanyi humu mnisaidie kuniambia, je msemaji wa timu au taasisi hivi ndivyo anavyotakiwa kutekeleza wajibu wake?

Maneno yenyewe ni kama haya yafuatayo:

" Kwanza huyo Manara ni mpuuzi kabisa na wa hovyo "
" Mtu anakaa uswahilini ataweza kushindana na mimi niishie Mbezi beach? "
" Mimi namiliki gari la kifahari ambalo yeye hana na hatoweza kuwa nalo "
" Isitoshe nina elimu kubwa ya masters degree ambapo yeye hata diploma tu tatizo "
" Nina uwezo sasa hata wa kuoa mwanamke wa kizungu kwa kuwa mimi ni wa kimataifa zaidi "
" Afisa habari gani kutwa anashinidia mihogo pale Magomeni Kagera? "

Hayo hapo juu ndiyo maneno ya msemaji wa Yanga aliyoyasema jana ktk press conference, ila kutokana na pengine hao waandishi kumwogopa au kumpotezea hakuna aliyeyasema au hata kuyazungumzia isipokuwa chombo kimoja tu cha Magic Fm kipindi cha jana usiku. Na nimeamka leo asubuhi hii nikijua kuwa wale waandishi niliowaona jana pale wangeandika hii kitu na kukemea kwa maslahi na maendeleo ya mpira wetu. Cha kushangaza, hakuna print media yoyote iliyoandika hivyo!

Kidume nimeamua kujilipua kama kawaida yangu. Na kwa wale mtakaodhani hizo kauli nilizoziweka hapo juu Jerry Muro hakuzisema, nawaombeni Muangalie Video Hapo chini

Na cha kuchekesha zaidi, hizo kauli chafu zote alizitoa baada tu ya kuulizwa kuwa je, anasemaje kuhusu malalamiko ya timu za Simba na Azam kuwa Yanga inapendelewa na TFF, baada ya TFF kuyafanyia haraka sana marekebisho ya wachezaji wa kigeni, yaliyowaruhusu wachezaji wote wageni waliokuwa na matatizo na taratibu za vibali vya kucheza ligi kuu kuanzia leo, wakati kabla ya mechi ya Simba na Azam klabu ya Simba ilihangaika huko huko TFF ili wachezaji wake Paul Kiongera na Brian Majwega wacheze lakini TFF ikaikatalia Simba tena hadi kwa vitisho?

Nimetema nyongo rasmi na nawaachieni intellectuals na academicians mliopo humu muweze kujadili zaidi, ila naiomba klabu ya Yanga iliangalie suala hili kwa umakini mkubwa mno hasa kwa huyu msemaji wao kwani akiachwa aendelee kuwa na hizi lugha zisizo na staha kuna siku mpira wetu utachafuka na hata kusababisha machafuko makubwa na hadi vifo.

Binafsi nimesikitika mno!​

Angalia Video Hapa




Comments

Popular posts from this blog

TAZAMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU WAKIVUNJA AMRI YA 6 NYUMA YA DARASA>>VIDEO HII HAPA>>