Wapenzi kupigana picha za utupu wakiwa faragha
Picha haijamaanisha makala hii..
Wapo watu ni wa ajabu sana kiasi kwamba mambo wanayofanya huwezi kuamini kuwa yanafanywa na mtu mwenye akili zake timamu.
Wapo watu ni wa ajabu sana kiasi kwamba mambo wanayofanya huwezi kuamini kuwa yanafanywa na mtu mwenye akili zake timamu.
Mbaya zaidi wengine ni watu wazima na familia zao lakini kwa ufyatu wao wanafanya mambo ya kijinga ambayo ni kinyume na maadili ya Kitanzania.
Kuna haka katabia ka' baadhi ya watu wawapo faraga kuwasha simu zao kisha kuwafotoa wapenzi wao wakiwa kama walivyozaliwa, mara nyingi nimekuwa nikijiuliza, hivi huu ni uungwana kweli?
Maana ninachojua picha ni kwa ajili ya kumbukumbu, sasa yule anayefikia hatua ya kumpiga picha mtu wake akiwa mtupu au wakati mwingine kumrekodi video chafu ni ili iweje?
Kwamba unatumia jitihada kubwa sana kuhakikisha unakuwa na picha za mpenzi wako kwenye simu yako akiwa mtupu, kwa matumizi yapi? Na kama ni kwa nia njema, kwa nini ufanye hivyo kwa kuvizia au kulazimisha?
Nauliza hivyo kwa sababu nimebaini hako kamchezo sasa hivi kameshamiri sana huko mtaani, imekuwa ni kama fasheni wakati ni jambo la aibu kabisa. Wapo wanaodhani kutokuwa na picha za wapenzi wao wakiwa watupu kwenye simu zao ni udhaifu mkubwa, za nini sasa?
Hii siyo sawa hata kidogo na mbaya zaidi waathirika wakubwa ni wanawake, baadhi kwa kujitakia. Nasema kwa kujitakia kwa sababu, kuna ambao wanaombwa tena kwa maneno matamu wapigwe picha na wapenzi wao halafu eti kwa kuwa wanawapenda wanapozi tena kwa mbwembwe.
Kwa nini ukubali kupigwa picha ukiwa mtupu? Hujaona hatari iliyo mbele yako ikiwa utakuwa umepigwa picha na mtu kisha akabaki nazo kwenye simu yake? Hujaona walioaibishwa baada ya kuachana kisha picha zao chafu kusambazwa mtandaoni? Huu siyo uungwana hata kidogo, ni ulimbukeni uliopitiliza!
Najua wapo ambao wanafanyiwa mchezo huo bila kujua. Mtu na mtu wake wako chumbani, jamaa anachukua simu yake, anajifanya anatuma ujumbe kisha anamfotoa mpenzi wake kwa siri. Au mwanamke baada ya kufanya mambo yao akapitiwa na usingizi, jamaa anamvizia kisha anamfotoa picha, hii siyo sawa!
Naomba niseme tu kwamba, endapo mpenzi wako anataka kukufotoa picha za utupu jua huyo hana mapenzi ya dhati kwako kwa kuwa si jambo la kiungwana. Anayefanya hivyo ni mbabaishaji asiye na nia nzuri na wewe.
Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati, hawezi kufanya kitendo hicho cha udhalilishaji kwa anayempenda.
Huenda mimi nakosea, labda nikuulize wewe msomaji wangu kwamba, wapenzi kupigana picha za utupu wakiwa faragha ni uungwana?
Comments
Post a Comment