Manyika Jr na Naima wapanga Kufunga ndoa, Aeleza Misukosuko Waliyopitia
Mlinda mlango wa Simba, Peter Manyika Jr na mchumba wake Naima wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.
Wawili hao wamepitia misukosuko mingi kwenye uhusiano wao ikiwa ni pamoja na kuwa kwenye hatari kuvunjika kwa uhusiano wao kutokana na shinikizo la wazazi na uongozi wa Simba.
Klabu ya Simba iliwahi kumuonya mchezaji huyo baada ya kuwashambulia mashabiki wa soka kwenye mtandao waliodai kuwa Naima ni chanzo cha kushuka kwa kiwango chake uwanjani.
Akiongea kwenye kipindi cha Uhondo cha EFM kinachoendeshwa na Dina Marious na Swebe, Jumatano hii, Manyika alisema ni mama yake ndiye aliyemvusha kwenye mapito hayo na anamchukulia kama shujaa wake.
Alisema maneno hayo yalimsumbua kisaikolojia na kuathiri mchezo wake uwanjani lakini mama yake alimsaidia na kumpa moyo.
Aliongeza kuwa baba yake, Peter Manyika pia alikuwa hajaupa baraka uhusiano wao lakini mama yake alimshawishi mume wake ampe support mwanae na kumwacha achague maisha yake mwenyewe hasa mwanamke wa kuwa naye.
Kuhusu tetesi kuwa alimpokonya Naima kwa Aslay wa Yamoto Band, Manyika alisema alimkuta msichana huyo akiwa single.
Bongo5
Comments
Post a Comment